Taasisi ya kimataifa ya uhudumiaji wa bidhaa na uchukuzi
wa bidhaa CILT yani THE CHARTERD INSTITUTE OF LOGISTIC AND TRANSPORT Tawi la Tanzania
imeandaa mkutano mkubwa nchini ambao utafanyika katika mkoa wa arusha tarehe 3
na 4 mwezi wa tatu mkutano wenye lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali wa
maswala ya usafirishaji na uchukuzi kujadili changamoto mbalimbli katika secta
hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kupata chai yenye lengo la kuchangisha fedha ambazo zitasaidia katika kuendesha mutano huo aliyekuwa waziri wa uchukuzi ambaye sasa ni waziri wa ushirikian wa Africa mashariki MH HARSON MWAKYEMBE amesema kuwa Tanzania kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa kama huu ni fursa ya kipekee ambayo nchi inatakiwa kujivunia na kuitumia kujitangaza kimataifa.
Aidha mwenyekiti wa CILT nchini Tanzania GEORGE
MAKUKE anesema kuwa kwa sasa katika secta ya usafirishaj wa bidha nchini
kumekuwa na watu ambao amewaita makanjanja ambao wamekuwa hawana weledi katika
kazi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi jambo ambalo amesema kuwa
linafaa kupigwa vita mara moja.
Katika hatua nyingine
mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo ndugu ZAKARIA HANSPOP akizngumza
katika hafla hiyo amewataka watanzania hususani wadau wa secta hiyo kujitoa
katika kuufadhili mkutano huo kwani una manufaa makubwa katika ukuaji wa secta
ya usafirishaji na uchukuzi nchini Tanzania
| Picha tatu za juu zikionyesha washiriki mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo |
No comments:
Post a Comment