Rais Jakaya Kikwete
anatarijiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya sheria nchini (Law Day) itakayofanyika Februari 4, 2015, katika viwanja vya mahakama vilivyopo mtaa wa Chimala jijini Dar es
salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Jaji Mkuu wa Tanzania
Mh. Othman Chande amesema kuwa
maadhimisho hayo kwa mwaka huu yanaongozwa na maudhui yasemayo “ Fursa ya kupata haki: wajibu wa Serikali,
Mahakama na wadau”.
Amesema kwa mara ya kwanza maadhimisho
hayo yataambatana na maonesho ya Wiki ya Shera yatakayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia
tarehe
30 Januari 2015 hadi tarehe 2 Februari 2015 .
Mh.Chande ameeleza kuwa maadhimisho
ya Siku ya Sheria nchini na maonesho ya Wiki ya Sheria yanaashiria mwanzo wa
shughuli za mahakama kwa mwaka 2015 na kufafanua kuwa kipaumbele kitatolewa
katika kupunguza mrundikano wa mashauri ya muda mrefu yaliyoko mahakamani na
kushughulikia mashauri yenye mvuto mkubwa kijamii,miradi mikubwa, uhujumu
uchumi, madawa ya kulevya, Biashara ndani na nje ya nchi na Rushwa.
Kuhusu maonesho hayo amesema
yanalenga kutoa elimu kwa wadau wa
sheria na huduma za kisheria kwa wananchi kuhusu Ufunguaji na uendeshaji wa
mashauri mbalimbali hasa mirathi, Utatuzi wa migogoro kwa njia ya suluhu, kueleza
mfumo mpya wa ulipaji wa tozo za kimahakama kwa njia ya benki, Kutoa msaada wa
kisheria, kutolewa vyeti vya mawakili, kupokea maoni na malalamiko kwa ajili ya
kuyatafutia ufumbuzi.
Ameeleza kuwa wadau
wakuu watakaoshiriki katika maonesho
hayo ni Mahakama, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka, Chuo cha Uongozi wa Mahakama-
Lushoto, Taasisi ya Mafunzo ya Uansheria kwa vitendo Tanzania na Tume ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora.
Wadau wengine ni
Taasisi zinazotoa msaada wa kisheria, TAKUKURU, Jeshi la Polisi, Magereza,
Chama cha Mawakili Tanganyika na Tume ya kurekebisha sheria.
Amesema pamoja na
maonesho hayo kutakuwa na matembezi maalum ya kuadhimisha Wiki ya Sheria tarehe
1 Februari 2015 yatakayoongozwa na Rais mstaafu wa awamu ya pili Mh. Ali Hassan
Mwinyi kuanzia Mahakama Kisutu kupitia barabara za Serena-Ohio, Gymkana –Obama Road,
Mahakama ya Biashara, Barabara ya Kivukoni, Sokoine , Railway, Nkurumah,
Lumumba na Mkunguni hadi Mnazi Mmoja.

No comments:
Post a Comment