Sikiliza Tone

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

www.missdemocrasiatz.com

www.missdemocrasiatz.com

TAN

TAN

DKT

DKT

Wednesday, 28 January 2015

WANANCHI WATAKIWA KUTOKATA MISITU YA ASILI NA KUCHIMBA MCHANGA HOVYO.

Na Abdulla Ali Maelezo-Zanzibar  .                                         
Naibu Waziri wa Kilimo na Maliasili Zanzibar Mhe. Mtumwa Kheir Mbarak amewataka wananchi kutokata misitu ya asili na kuchimba mchanga ovyo kwani ndizo sababu zinazopelekea mabadiliko ya Tabianchi.

Hayo ameyaeleza katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi Unguja wakati akijibu swali la mwakilishi wa Jimbo la Wawi Mhe. Saleh Nassor Juma.

Mhe. Mtumwa amesema ukataji wa misitu ya asili pamoja na uchimbaji mchanga ovyo husababisha kukosekana kwa mvua za misimu na kuathiri maisha ya wakulima na wananchi kwa ujumla.

Amesema ikiwa wananchi wataendelea kukata misitu ya asili hususan mikoko ambayo huzuia upepo wa Bahari na kupandisha kina cha maji, kutapelekea Visiwa vya Zanzibar kukatika vipandevipande na maji kujaa hadi katika makaazi ya watu kama ilivyo hivi sasa kwa baadhi ya vijiji hapa zanzibar.  

“Na athari za ziada zitafuata baadae ikiwa wataendelea kukata hasa mikoko ambayo inazuia upepo wa Bahari na kupandisha kina cha maji, matokeo yake visiwa vitakatika vipande vipande na maji yatapanda mpaka viamboni (katika makaazi ya watu) na mfano hai hayo sasa yanatokea katika vijiji vya Jozani, Mziwanda, Koowe na kwengine kwingi”, alieleza Naibu Waziri Mtumwa. 

Aidha ametanabahisha kuwa Serikali imechukua juhudi mbalimbali katika kuhakikisha kwamba athari za mabadiliko hayo zinapungua, miongoni mwa juhudi hizo ni kuanzishwa vikundi mbalimbali vya jamii husika kwa matakwa yao wenyewe kutunza misitu ya asili iliopo katika maeneo yao wanayoishi Unguja na Pemba, Udhibiti wa msumeno wa moto kutotumika mpaka kwa ruhusa na kibali maalumu.

No comments:

Post a Comment