Sikiliza Tone

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

www.missdemocrasiatz.com

www.missdemocrasiatz.com

TAN

TAN

DKT

DKT

Wednesday, 9 March 2016

RAIS MAGUFULI AMKARIBISHA RAIS WA VIETNAM, MHE. TRUONG TAN SANG IKULU, DAR ES SALAAM

  • VIDEO YA RAIS MAGUFULI ALIVYOMJULIA HALI MAALIM SEIF NA SIKILIZA NINI WAWILI HAO WALICHOONGEA
  • Je ukimfumania mwenza wako unaweza kumsamehe?
  • MAMA JANETH MAGUFULI AKIMKARIBISHA MKE WA RAIS WA VIETNAM, BI. MAI THI HANH OFISINI KWAKE.
  • RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS TUONG WA VIETNAM LEO
  • RAIS DKT. MAGUFULI AMTEMBELEA NA KUMJULIA HALI MAALIMU SEIF SHARIF HAMAD.
  • UMOJA WA MATAIFA WANAWAKE WAZINDUA KUNDI LA ‘HEFORSHE’, LENGO KUWEKA USAWA WA KIJINSIA
  • Kichupa cha leo UMEBADILIKA - Daddy Face
  • MAOMBI MAALUM YA KUMWOMBEA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI NA SERIKALI YAKE YAFANYIKA JIJINI MBEYA
  • WIKI SASA TOKA DADA YETU JASSIE AKUTWE NA UMAUTI HAPA NI TASWIRA YA JINSI WATU WALIVYOJITOKEZA KWA WINGI KUAGA MWILI MURCH 2 HUKO YORKERS NY.
  • MKUU WA MKOA WA MTWARA MH. HALIMA DENDEGU AZINDUA RASMI SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2016 KATIKA UWANJA WA MASHUJAA.
  • Hospitali za rufani, mikoa ni majanga.
  • Misa Takatifu ya kumbukumbu ya kijana wao mpendwa James Luhanga Jr
  • HAPPY BIRTHDAY
  • Mzee yusuf, watulize wake zako!
  • BODI YA BARABARA MKOA WA LINDI YAANZA VIKAO
  • MWANARIADHA WA TANZANIA ALPHONCE FELIX AREJEA NCHINI BAADA YA KUSHIKA NAFASI YA TATU KATIKA MASHINDANO YA LAKE BIWA MARATHONI YA NCHINI JAPAN
  • Maalim Seif: Niko fiti
  • MECHI ZA LIGI YA TANZANIA BARA ZITAKAZOCHEZWA LEO JUMATANO HIZI HAPA
  • Mawaziri wanne wa JPM matatani
  • TAASISI YA TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA) YAANDAA KONGAMANO LA KUTOA AHADI YA UWIANO SAWA WA KIJINSIA
  • DONDOO ZA MAGAZETI
  • WATU WATATU WAFARIKI NA ZAIDI YA 16 WAJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI MATATU BARABARA YA MANDELA JIJINI DAR LEO ASUBUHI
  • JE WAJUA TIMU YA TOTO AFRICANS YA JIJINI MWANZA NDIYO TIMU MASKINI KULIKO ZOTE LIGI KUU NCHINI?
RAIS MAGUFULI AMKARIBISHA RAIS WA VIETNAM, MHE. TRUONG TAN SANG IKULU, DAR ES SALAAM
Posted: 09 Mar 2016 12:56 PM PST
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kulia) akiwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya ziara yake ya kikazi yenye kuendeleza mahusiano baina ya Tanzania na Vietnam. 
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (mwenye gauni jekundu) akipokea ua toka kwa mtoto mara alipowasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 akiwa ameambatana na mmewe kwa ajili ya ziara yake ya kikazi yenye kuendeleza mahusiano baina ya Tanzania na Vietnam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kulia) akimkaribisha mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang mara alipowasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kulia) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye koti la drafti) mara alipowasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016. Wa kwanza kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli. 
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa tatu kulia) akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (wa tatu kushoto) mara alipowasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kulia) pamoja na Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakipanda jukwaani kwa ajili ya kuimbiwa nyimbo za taifa kabla ya kukagua gwaride 9 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) pamoja na Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakiwa jukwaani kwa ajili ya kuimbiwa nyimbo za taifa kabla ya kukagua gwaride 9 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang(mwenye tai nyekundu) akikagua gwaride mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016. 
Umati wa watu wakiwa ndani Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya kumpokea Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang aliyewasili jana kwa ajili ya ziara yake ya kazi nchini Tanzania. 
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kushoto) pamoja na mkewe mama
Mai Thi Hanh (mwenye gauni jekundu) wakiingia ndani ya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa mara ya kwanza kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye kukuza uhusiano baina ya Tanzania na Vietnam 
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (mwenye gauni jekundu) akisalimiana na akina mama waliompokea mara alipotembelea katika ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli 9 Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam. 
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh akisaini kitabu cha wageni mara alipowasili katika ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli (kulia) 9 Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam. 
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh pamoja na Mama Janeth Magufuli wakifurahia jambo 9 Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam. 
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (kushoto) akifurahia zawadi ya kinyago cha kuchonga alichokabidhiwa na mwenyeji wake mama Janeth Magufuli kama zawadi 9 Machi, 2016 katika ofisi za Mke wa Rais Jijini Dar es Salaam. 
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (kushoto) akimpa zawadi mama Janeth Magufuli ikiwa shukurani yake mara alipotembelea katika ofisi yake 9 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake mama Mai Thi Hanh mara baada ya kutembelea katika ofisi hiyo leo 9 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (mwenye gauni jekundu) akipata maelezo kuhusu nyaraka mbalimbali ziliko katika Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam leo 9 Machi, 2016. 
VIDEO YA RAIS MAGUFULI ALIVYOMJULIA HALI MAALIM SEIF NA SIKILIZA NINI WAWILI HAO WALICHOONGEA
Posted: 09 Mar 2016 12:49 PM PST
Je ukimfumania mwenza wako unaweza kumsamehe?
Posted: 09 Mar 2016 10:40 AM PST

MAMA JANETH MAGUFULI AKIMKARIBISHA MKE WA RAIS WA VIETNAM, BI. MAI THI HANH OFISINI KWAKE.
Posted: 09 Mar 2016 08:49 AM PST
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (mwenye gauni jekundu) akisalimiana na akina mama waliompokea mara alipotembelea katika ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli 9 Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (mwenye gauni jekundu) akisalimiana na wacheza ngoma mara alipotembelea katika ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli 9 Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh akisaini kitabu cha wageni mara alipowasili katika ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli (kulia) 9 Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (kushoto) akifurahia zawadi ya kinyago cha kuchonga alichokabidhiwa na mwenyeji wake mama Janeth Magufuli kama zawadi 9 Machi, 2016 katika ofisi za Mke wa Rais Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (kushoto) akimpa zawadi mama Janeth Magufuli ikiwa shukurani yake mara alipotembelea katika ofisi yake 9 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO).
RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS TUONG WA VIETNAM LEO
Posted: 09 Mar 2016 06:31 AM PST
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimkaribisha Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, kwa ajili ya mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang na ujumbe wake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Zakia Meghji na Waziri Mahiga.
  Rais Truong wa Vietnam akimsifia jambo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akati akimuaga baada ya mazungumzo yake na Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete (kulia)
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang na ujumbe wake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Zakia Meghji na Waziri Mahiga na kulia ni Dk. Asha-Rose Migiro.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa na ujumbe wake katika mazungumzo hayo 
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Rais Truong baada ya mazungumzo yao. Kulia ni Dk. Asha-Rose Migiro na Abdulrahman Kinana. na Kushoto ni Waziri Mahiga.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Rais Truong baada ya mazungumzo yao. Walioketi kulia ni Dk. Asha-Rose Migiro na Abdulrahman Kinana. na Kushoto ni Waziri Mahiga. Na waliosimama ni baadhi ya viongozi waandamizi walioshiriki katika mazungumzo kwa upande wa Mwenyekiti wa CCM Kikwete na wa upande wa Rais Truong.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitoka na mgeni wake, Rais Truong wa Vietnam baada ya mazungumzo yao. 
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiagana na mgeni wake, Rais wa Truong wa Vietnam baada ya mazungumzo yao
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiagana na mgeni wake, Rais wa Truong wa Vietnam baada ya mazungumzo yao. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
 Rais Truong wa Vietnam akiagana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, baada ya mazungumzo yake na Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete (kulia)
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimsindikiza Rais Truong wa Vietnam kwenda kupanda gari
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimsindikiza Rais Truong wa Vietnam kwenda kupanda gari
 Rais Truong wa Vietnam akiwaaga wananchi waliokuwa nje ya jengo la Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba kabla ya kuondoka
  Rais Truong wa Vietnam akiwashukuru wananchi waliokuwa nje ya jengo la Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba kabla ya kuondoka
 Rais wa Truong wa Vietnam akimuaga mwenyeji wake, Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kabla ya kuondoka
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimpungia mkono kumtakia ziara njema, Rais Truong wakati wakiondoka na msafara wake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam
 "Naam, Nadhani ugeni wetu tumeupokea na kuuaga vizuri", Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimweleza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baada ya Rais Truong wa Vietnam kuondoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba. 
 "NIMEWA-MISS SANA"Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwasalimia waandishi wa habari waliofika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kuchukua taarifa za ujio wa Rais Truong 
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na waandishi wa habari kuhusu yaliyojiri katika mazungumzo yake na Rais Truong wa Vietnam.   Aliwaambia kwamba kikubwa walichozungumza na mgeni wake ni kuhusu mahusiano kati ya CCM na nchi hiyo ya Vietnam, hasa ikizingatiwa kwamba, Nchi hiyo ilishiriki kwa namana moja au nyingine katika harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika na harakati nyingine za ukombozi wa Mwafrika hasa Watanzania enzi za Baba wa Taifa Hatari Mwalimu Nyerere.. 
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimkaribisha Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, kwa ajili ya mazungumzo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya faragha ofisini kwake na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, kwa ajili ya mazungumzo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini
 Waziri wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga akizungumza na Katibu wa NEC anayeshughulikia Uchumi na Fedha wa CCM, Zakiah Megji wakati wa mazungumzo ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na mgeni wake, Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
 Katibu wa NEC, Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akiwa na Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatibu wakati wa mazungumzo hayo ya Kikwete na Rais wa Vietnam. Kulia Ni Kaim Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Shaka Hamidu Shaka
 Viongozi na Maofisa wa CCM wakiwa kwenye mazungumzo hayo
PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
RAIS DKT. MAGUFULI AMTEMBELEA NA KUMJULIA HALI MAALIMU SEIF SHARIF HAMAD.
Posted: 09 Mar 2016 06:24 AM PST

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam. Maalim Seif aliruhusiwa kutoka hospitalini jana na hali yake inaendelea vizuri.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam. Maalim Seif amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumjulia hali  na kusema kuwa hali yake ya kiafya inaimarika siku baada ya siku.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam mara baada ya kumjulia hali jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  



UMOJA WA MATAIFA WANAWAKE WAZINDUA KUNDI LA ‘HEFORSHE’, LENGO KUWEKA USAWA WA KIJINSIA
Posted: 09 Mar 2016 06:21 AM PST
DSC_1297
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa hotuba katika mdahalo kuhusu wanawake na uzinduzi wa Kundi la `HeForShe`.
DSC_1248Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt (wa kwanza kulia), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake nchini, Anna Collins-Falk

Umoja wa Mataifa Wanawake (UN Women) nchini umefanya uzinduzi wa kundi la mshikamano la Kimataifa linalohusisha wanaume na wavulana lililo na malengo ya kuhakikisha kunapatikana usawa wa kijinsia baina ya wanaume na wanawake ‘HeForShe’.
Akizindua kundi hilo, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez alisema usawa kijinsia ni haki ya kila binadamu na kupitia kundi hilo ni wajibu wa kila mwanaume na mvulana kusaidia kupatikana kwa usawa kwa wanaume na wanawake katika maeneo yote ambayo yanaonekana kuwa na upendeleo kwa upande mmoja.
“Usawa wa kijinsia sio tu suala la wanawake pekee, ni suala la haki za binadamu ambalo hutuathiri sisi sote. Usawa wa kijinsia sio tu kuwawezesha wanawake, lakini pia huweka huru watu kutoka katika ubaguzi uliowekwa kijamii na majukumu ya kijinsia,” alisema Rodriguez.
Awali Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt alieleza kuwa usawa wa kijinsia unahusisha pia katika kusimamia shughuli mbalimbali ikiwepo za nyumbani kwa wanaume na wanawake kushirikiana kuzifanya kwa pamoja.
Alisema ni muhimu kwa jamii kuelewa kuwa ni jambo lenye maana kuwepo kwa usawa wa kijinsia ili wanawake nao waweze kusaidia shughuli za maendeleo kwa familia na taifa kwa ujumla.
“Usawa uwepo katika sehemu zote hata kazi za nyumbani zifanyike kwa pamoja … ni muhimu kwa mama, baba na kijana kuwepo kwa usawa wa kijinsia kwa watu wote,” alisema Bi. Rangnitt.
Siku ya Wanawake kwa mwaka huu kidunia imekuwa na kauli mbiu ya kimataifa isemayo ‘Dunia 50-50 Ongeza Jitihada kwa ajili ya Usawa wa Kijinsia’ na kitaifa kaulimbiu imekuwa ni ’50-50 ifikapo 2030 Tuongeze Jitihada’.
DSC_1245Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizindua Kundi la Mshikamano la `HeForShe`.
DSC_1259
Mdahalo ukiendelea, (wa kwanza kulia) Katibu Mkuu wa Bazara Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng`i Issa, Kiongozi wa Timu ya Umoja wa Mataifa wa Wanawake ya Uwezeshaji Kiuchumi, Mehjabeen Alarakhia na Mshauri wa Jinsia na Maendeleo, Edward Mhina.
DSC_1290Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa hotuba katika mdahalo kuhusu wanawake na uzinduzi wa Kundi la `HeForShe`.
DSC_1237Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt.akitoa hotuba kuhusiana Siku ya Wanawake.
DSC_1226Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake nchini, Anna Collins-Falk
DSC_1216Mshereheshaji wa mdahalo huo, Usu Mallya
DSC_1182Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake nchini, Anna Collins-Falk akikata keki ya kusherekea Siku ya Wanawake Duniani, Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez.
DSC_1176 DSC_1174
Kichupa cha leo UMEBADILIKA - Daddy Face
Posted: 09 Mar 2016 05:30 AM PST
MAOMBI MAALUM YA KUMWOMBEA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI NA SERIKALI YAKE YAFANYIKA JIJINI MBEYA
Posted: 09 Mar 2016 04:40 AM PST
Baadhi ya maaskofu kutoka makanisa mbalimbali Mkoani Mbeya wakiwa wamshika Picha ya Rais  na ramani ya Tanzania wakati wa maombi maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mkapa jijini Mbeya.
Picha ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ikiwa imeshikwa na maaskofu wa makanisa mbalimbali Mkoani Mbeya kwa ajili ya kufanya maombi maalumu kwa ajili ya rais na serikali yake katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya
Muongozaji Mkuu wa Maombi ya kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli ,Askofu Dkt  Charles Gadi wa kanisa la The City of refuge Church  yenye makao makuu jijini Dar es salaam akizungumza na waumini walioshiriki katika maombi hayo katika ukumbi wa Mkapa .
Askofu Dkt  Charles Gadi wa kanisa la The City of refuge Church  yenye makao makuu jijini Dar es salaam akizungumza na waumini walioshiriki katika maombi ya kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake  katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya March 8 mwaka huu. .
Baadhi ya waumini walioshiriki Maombi Maalum ya Kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake yaliyoandaliwa na Jukwaa la wakristo Mkoani Mbeya kwa kushirikiana na Askofu Mkuu wa Kanisa la The City of refuge Church Dkt Charles Gadi katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya March 8 mwaka huu.
Baadhi ya maaskofu  na waumini kutoka jukwaa la Wakristo Mkoa wa Mbeya wakiwa katika maombi maalumu ya kumwombea Rais Dkt  John Pombe Magufuli na serikali yake katika ukumbi wa Mkapa jijni Mbeya Machi 8 mwaka huu na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali mkoani humo.
kwaya zikiendelea kutumbuiza katika maombi hayo ya kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya Machi 8 mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyilembe Munasa  kushoto pamoja na Askofu Charles Gadi mwenye miwani  wakiwa katika maombi maalum ya kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Maombi yakiendelea....
Baadhi ya viongozi wa makanisa mbalimbali mkoani mbeya wakiwa katika maombi maalumu ya kumwombea Rais Dkt Maguli na serikali yake .
Picha na Jamiimojablogu Mbeya.....
WIKI SASA TOKA DADA YETU JASSIE AKUTWE NA UMAUTI HAPA NI TASWIRA YA JINSI WATU WALIVYOJITOKEZA KWA WINGI KUAGA MWILI MURCH 2 HUKO YORKERS NY.
Posted: 09 Mar 2016 03:30 AM PST
TASWIRA YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU JESSIE CHIUME KWA SAFARI YAKE YA MILELE TANZANIA, SHUGHULI HIZO ZA KUAGA MWILI ZILIFANYIKA FLYNN MEMORIAL HOME YONKERS. NY, SIKU YA JUMATANO MURCH 2.  NA KUSAFIRISHWA ALHAMIS MARCH 3, NA MAZISHI KUFANYIKA MARCH 5, MAKABURI YA KINONDONI DAR-ES-SALAAM. KWA PICHA ZAIDI NENDA SOMA ZAIDI.
Hapa ni ndugu wa marehemu wakishindwa kujizuia wakati wa kuaga mwili wa ndugu yao, msiba wa Jessie uliwagusa wengi sana ukiacha ndugu na Watanzani hata wafanyakazi wenzake pia waliguswa na walishindwa kujizuia kutoa machozi wakati wa kuaga mwili wa marehemu. Watu walijitokeza kwa wingi hadi kukosa nafasi na kisha kuamishiwa kwechumba kingine na kufatilia misa kwa njia ya TV kubwa ya ukutani.
Hapa ni mume wa marehemu akiwa mwenye majonzi
Sonia mdogo wa marehemu akiwa hana la kusema wala kuamini kuwa anachokiona ni kweli kimetokea.
Kaka mkubwa wa marehemu bwana Michael Chiume
Mdogo wa marehemu Nathan Chiume
Mdogo mwingine wa marehemu akiwa pembeni na mchumba wake
Wafanya kazi wenzake wakiwa na nyuso za majonzi wakifarijiwa na Dr, Temba mweka hazina wa New York Tanzania Communities.
Hapa ni familia ya marehemu  kutoka kulia ni Nathan, Michael, mama wa marehemu, Sonia na mume wa marehemu.